"Watu wangelijua uzuri wa maneno yetu, wangelitufuata"
Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Leo hii nchini Burundi kimefanyika kikao cha kielimu na kiroho kiitwacho “Asubuhi ya Kiroho” ambacho kilibeba mada kuu isemayo: “Juhudi za Imam Jaafar Sadiq (a.s) katika Kuelimisha Watu.”
Darsa hiyo ilijikita katika kubainisha juhudi kubwa alizofanya Imam Jaafar Sadiq (a.s) katika kuwaelimisha watu kuhusu masuala ya dini, kueneza maadili mema, pamoja na kuimarisha elimu sahihi ya Kiislamu kwa vizazi mbalimbali.
Aidha, kikao hicho kiliashiria umuhimu wa kuhuisha mafundisho ya Ahlul-Bayt (a.s) kwa kurejea kwenye maneno ya Imam Jaafar Sadiq (a.s) aliposema:
"لو علموا الناس محاسن كلامنا لتبعون"
“Watu wangelijua uzuri wa maneno yetu, wangelitufuata.”
Kwa mujibu wa waandaaji, darsa hizi za Asubuhi ya Kiroho zinaendelea kufanyika mara kwa mara zikiwa ni fursa ya kuimarisha uhusiano wa waumini na mafundisho ya Qur’an na Ahlul-Bayt (a.s).
Your Comment